MIKEBE: LEO NI HUKU, KESHO NI KULE!Karibu kwenye soko la siasa za Kenya, ambako bidhaa hubadilika bei, wauzaji hubadilisha maduka, na misimamo ya kisiasa hubadilika kulingana na upepo unaovuma!
Wale waliokuwa jana mstari wa mbele kupinga uongozi wa William Ruto leo wamegeuka kuwa mabalozi wake wakuu. Wengine wamebadilisha kambi, wengine wamebadilisha lugha, na wengine wamejikuta wakieleza kwa nini kile walichopinga jana ndicho wanachokisifu leo.
ODM nayo inakabiliwa na mtihani wa uongozi, umoja na mwelekeo wa kisiasa katika kipindi cha mpito baada ya kifo cha Raila Odinga.
Lakini huku wanasiasa wakibadilishana misimamo na kupanga mikakati ya 2027, mwananchi wa kawaida ana maswali ambayo hayawezi kujibiwa kwa hotuba za majukwaani.
Maji safi yako wapi? Ajira ziko wapi? Biashara ndogo zitawezaje kuhimili mzigo wa kodi? Wazazi watawezaje kumudu gharama za elimu? Na ni lini maendeleo yataanza kuonekana moja kwa moja kwenye mifuko na maisha ya wananchi?
Ni kweli, barabara, masoko, viwanja vya michezo na nyumba ni sehemu ya maendeleo. Lakini maendeleo hayawezi kupimwa kwa ukubwa wa majengo pekee; lazima yapimwe pia kwa ubora wa maisha ya wananchi.
Hapo ndipo tunapokumbuka zile KIMBO, COWBOY na BLUE BAND za zamani. Makopo ambayo yalikuwa na majina makubwa, rangi za kuvutia na matangazo ya kuvutia, lakini siku yalipoisha yaliyomo, kilichobaki ni kopo tu!
Katika siasa, jina la chama, ukubwa wa mkutano na idadi ya wafuasi si mbadala wa misimamo, sera na uwajibikaji.
Mwananchi anahitaji viongozi wenye msimamo, si misimamo inayobadilika kila upepo wa kisiasa unapovuma.
MIKEBE! LEO NI HUKU, KESHO NI KULE!
Swali si nani amehama kambi. Swali ni nani bado amesimama na mwananchi?
#MIKEBE #SiasaZaKenya #Uchaguzi2027 #Uwajibikaji
KWAELA: https://www.facebook.com/share/p/1KhTaLXnx5/


















